Thursday, July 31, 2014
On 1:56 PM by alamagroup No comments
TAMBUA FURSA
Benki ya Azania inakusudia kuwa benki
inayoongoza katika kutoa huduma za kibenki
kwa wateja wadogo na wa kati.
Hatua muhimu za kuzingatia!
1. Nyambulisha na uainishe mradi unaotaka
kufanya kwa msingi wa wazo linalotekelezeka
2. Fursa ya biashara hutokana na yafuatayo
a. Tathmini ya wazo lako la biashara.
b. Tathmini ya kina ya mahitaji ya soko ambalo
biashara yako italenga.
c. Tathmini ya kina ya bidhaa zako na huduma
zako.
d. Tathmini ya kina na jinsi bidhaa yako/huduma
yako itakavyokidhi mahitaji ya soko ulilolenga
e. Fikiria na ufafanue walengwa/watumiaji wa
bidhaa au huduma zako.
f. Tathimini taratibu za kisheria na kiutawala
kuhusu biashara unayotaka kuanzisha.
3. Angalia ushindani uliopo sokoni (husisha
yafuatayo)
a. Angalia na uorodheshe biashara nyingine
zinazotoa huduma/bidhaa kama unazotaka
kutoa wewe.
b. Angalia na ujiulize kama wapo washindani
wengine wapya wanaotaka kuingia kwenye
biashara hiyo hiyo unayokusudia.
c. Jiulize changamoto zilizopo na vikwazo vilivyopo
(kisheria, kimtaji, au vinginevyo) vinavyoweza
kuzuia biashara nyingine zinazofanana na
biashara yako kuanzishwa.
d. Jiulize na uorodheshe upekee wa
bidhaa/huduma zako (jiulize sababu za
kumfanya mtu ahitaji bidhaa/huduma yako
badala ya bidhaa/huduma nyingine zilizopo
sokoni)
4. Angalia uwezekano wa biashara yako
kuendelea na kukua (ujibu yafuatayo)
a. Utawafikiaje walengwa wa biashara yako (Ni
kwa vipi walengwa wako watajua kuhusu bidhaa
na huduma zako)?
b. Utasambazaje/ fikishaje bidhaa/huduma zako
(Bidhaa zako zitafikaje kwa wauzaji wa rejareja
au huduma zako zitafikaje kwenye maeneo
uliyokusudia na maeneo hayo ni yapi)?
c. Nini makadirio yako ya wafanyakazi unaohitaji
kwa miaka miwili ya kazi (wafanyakazi wangapi
utahitaji mwaka wa kwanza, na wangapi utahitaji
mwaka wa pili)?
d. Unahitaji ufanye nini ili biashara yako ipate faida
na itachukua muda gani kuwa na faida?
e. Nini matarajio yako ya mapato na matumizi kwa
miaka 4 ya kazi (ni mapato na matumizi kiasi
gani katika mwaka wa kwanza, mwaka wa pili,
wa tatu na wa nne)?
f. Unahitaji mtaji wa kiasi gani (kiasi gani cha
fedha unachohitaji kuwekeza) katika mwaka wa
kwanza,wa pili, wa tatu na wa nne ili kuendesha
biashara yako?
g. Utawezaje kupata kiasi hicho cha mtaji? Je ni
kwa kuanza kuweka akiba katika benki au
kuomba mkopo na kwa gharama gani?. Je
mchango wako katika mtaji ni kiasi gani?
h. Je mradi wako unaweza ukabeba gharama
zinazotakiwa kiundeshaji na bado ukazalisha
faida?
5. Uzoefu wako katika ujasiriamali na
uwajibikaji.
a. Tathmini kiwango chako cha elimu na uzoefu
wako unaohusiana na wazo lako la biashara na
mahusiano uliyo nayo na wadau muhimu ki-
sekta wewe kama mjasiriamali.
b. Tathmini kuhusu wataalam wa fani mbalimbali
ambao utahitaji kuwatumia katika maeneo
ambayo wewe si mtaalam wala mzoefu ili
kufanikisha uanzishaji na uendeshaji wa biashara
yako.
c. Kwa ufupi tathmini nia/malengo yako ya
kutimiliza kuanza na kukua kwa biashara
ukizingatia muda utakaotumia kupanga, muda
unaokusudia kutumia katika mradi, kiwango cha
fedha za kwako mwenyewe unachoridhia
kuweka katika mradi n.k.
Subscribe to:
Comments (Atom)